Zaburi 99:6-9
Zaburi 99:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mose na Aroni walikuwa makuhani wake; Samueli alikuwa miongoni mwa waliomlilia. Walimlilia Mwenyezi-Mungu naye akawasikiliza. Alisema nao katika mnara wa wingu; waliyazingatia matakwa yake na amri alizowapa. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, wewe uliwasikiliza; kwao ulikuwa Mungu mwenye kusamehe, ingawa uliwaadhibu kwa makosa yao. Msifuni Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu; abuduni katika mlima wake mtakatifu! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni mtakatifu.
Zaburi 99:6-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Musa na Haruni walikuwa makuhani wake, Na Samweli pia ni miongoni mwa walioliitia jina lake, Walimlilia BWANA naye akawaitikia; Akasema nao katika nguzo ya wingu. Wakashika shuhuda zake na amri aliyowapa. Ee BWANA, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu; Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe Ingawa uliwapatiliza matendo yao. Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu.
Zaburi 99:6-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake, Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake, Walipomwita Bwana aliwaitikia; Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao. Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa. Ee BWANA, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu; Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe Ingawa uliwapatiliza matendo yao. Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana BWANA, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
Zaburi 99:6-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Musa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita BWANA, naye aliwajibu. Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; walizishika sheria zake na amri alizowapa. Ee BWANA, wetu, ndiwe uliyewajibu, kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe, ingawa uliadhibu matendo yao mabaya. Mtukuzeni BWANA Mungu wetu, mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana BWANA Mungu wetu ni mtakatifu.