Zaburi 98:1-3
Zaburi 98:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu! Mkono wake hodari, mkono wake mtakatifu umempatia ushindi. Mwenyezi-Mungu ameonesha ushindi wake; ameyadhihirishia mataifa uwezo wake wa kuokoa. Amekumbuka fadhili na uaminifu wake kwa Waisraeli. Pande zote za dunia zimeuona ushindi wa Mungu wetu.
Zaburi 98:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kulia, Na mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. BWANA ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
Zaburi 98:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. BWANA ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
Zaburi 98:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mwimbieni BWANA wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu; kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu umemfanyia wokovu. BWANA ameufanya wokovu wake ujulikane na amedhihirisha haki yake kwa mataifa. Ameukumbuka upendo wake na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli; miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.