Zaburi 96:7-9
Zaburi 96:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima, enyi jamii zote za watu; naam, kirini utukufu na nguvu yake. Lisifuni jina lake tukufu; leteni tambiko na kuingia hekaluni mwake. Mwabuduni Mwenyezi-Mungu katika patakatifu pake; tetemekeni mbele yake ee dunia yote!
Zaburi 96:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu, Mpeni BWANA utukufu na nguvu. Mpeni BWANA utukufu wa jina lake, Leteni sadaka, na mwingie katika nyua zake. Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu, Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
Zaburi 96:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu, Mpeni BWANA utukufu na nguvu. Mpeni BWANA utukufu wa jina lake, Leteni sadaka mkaziingie nyua zake. Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu, Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
Zaburi 96:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mpeni BWANA, enyi jamaa za mataifa, mpeni BWANA utukufu na nguvu. Mpeni BWANA utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake. Mwabuduni BWANA katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake.