Zaburi 96:1-4
Zaburi 96:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya! Mwimbieni Mwenyezi-Mungu, ulimwengu wote! Mwimbieni Mwenyezi-Mungu na kulisifu jina lake. Tangazeni kila siku matendo yake ya wokovu. Yatangazieni mataifa utukufu wake, waambieni watu wote matendo yake ya ajabu. Maana Mwenyezi-Mungu ni mkuu, anasifika sana; anastahili kuheshimiwa kuliko miungu yote.
Zaburi 96:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Mwimbieni BWANA, nchi yote. Mwimbieni BWANA, lisifuni jina lake, Tangazeni wokovu wake kila siku. Wahubirieni mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana. Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
Zaburi 96:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Mwimbieni BWANA, nchi yote. Mwimbieni BWANA, libarikini jina lake, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku. Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana. Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
Zaburi 96:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mwimbieni BWANA wimbo mpya; mwimbieni BWANA dunia yote. Mwimbieni BWANA, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. Tangazeni utukufu wake katika mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.