Zaburi 94:1-7
Zaburi 94:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu mwenye kulipiza kisasi, ewe Mungu mlipiza kisasi, ujitokeze! Usimame, ee hakimu wa watu wote; uwaadhibu wenye kiburi wanavyostahili! Waovu wataona fahari hata lini? Watajisifia mpaka lini, ee Mwenyezi-Mungu? Hata lini waovu watajigamba kwa maneno? Waovu wote watajivuna mpaka lini? Wanawaangamiza watu wako, ee Mwenyezi-Mungu, wanawakandamiza hao walio mali yako. Wanawaua wajane na wageni; wanawachinja yatima! Wanasema: “Mwenyezi-Mungu haoni, Mungu wa Yakobo hajui!”
Zaburi 94:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, Mungu wa kisasi, Mungu wa kisasi, uangaze, Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze, Uwape wenye kiburi stahili zao. BWANA, hadi lini wasio haki, Hadi lini wasio haki watashangilia? Je! Wote watendao uovu watatoa maneno, Na kusema majivuno, na kufanya kiburi? Ee BWANA, wanawaponda watu wako; Wanautesa urithi wako; Wanamwua mjane na mgeni; Wanawaua yatima. Nao husema, BWANA haoni; Mungu wa Yakobo hatambui.
Zaburi 94:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, Mungu wa kisasi, Mungu wa kisasi, uangaze, Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze, Uwape wenye kiburi stahili zao. BWANA, hata lini wasio haki, Hata lini wasio haki watashangilia? Je! Wote watendao uovu watatoa maneno, Na kusema majivuno, na kufanya kiburi? Ee BWANA, wanawaseta watu wako; Wanautesa urithi wako; Wanamwua mjane na mgeni; Wanawafisha yatima. Nao husema, BWANA haoni; Mungu wa Yakobo hafikiri.
Zaburi 94:1-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee BWANA, ulipizaye kisasi, Ee Mungu ulipizaye kisasi, uangaze sasa. Ee Mhukumu wa dunia, inuka, uwalipize wenye kiburi kama wanavyostahili. Ee BWANA, hadi lini waovu, hadi lini waovu watashangilia? Wanamimina maneno ya kiburi, watenda maovu wote wamejaa majivuno. Ee BWANA, wanawaponda watu wako; wanawatesa walio urithi wako. Wanamchinja mjane na mgeni, na kuwaua yatima. Nao husema, “BWANA haoni, Mungu wa Yakobo hafahamu.”