Zaburi 90:2-5
Zaburi 90:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Kabla ya kuwapo milima, kabla hujauumba ulimwengu; wewe ndiwe Mungu, milele na milele. Wamwambia binadamu, “Rudi mavumbini!” Naye binadamu hurudi mavumbini alimotoka! Kwako miaka elfu ni kama siku moja tu, ni kama jana ambayo imekwisha pita; kwako ni kama mkesha mmoja wa usiku! Wawafutilia mbali watu kama ndoto! Binadamu ni kama nyasi zinazochipua asubuhi
Zaburi 90:2-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu. Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu. Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku. Wawafutilia wanadamu mbali kama ndoto, wao ni kama majani yameayo asubuhi.
Zaburi 90:2-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu. Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu. Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku. Wawagharikisha, huwa kama usingizi, Asubuhi huwa kama majani yameayo.
Zaburi 90:2-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kabla ya kuzaliwa milima au hujaumba dunia na ulimwengu, wewe ni Mungu tangu milele hata milele. Huwarudisha watu mavumbini, ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.” Kwa maana kwako miaka elfu ni kama siku moja iliyokwisha pita, au kama kesha la usiku. Unawatowesha wanadamu katika usingizi wa kifo, nao ni kama majani machanga ya asubuhi