Zaburi 90:1-4
Zaburi 90:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Bwana, tangu vizazi vyote, wewe umekuwa usalama wetu. Kabla ya kuwapo milima, kabla hujauumba ulimwengu; wewe ndiwe Mungu, milele na milele. Wamwambia binadamu, “Rudi mavumbini!” Naye binadamu hurudi mavumbini alimotoka! Kwako miaka elfu ni kama siku moja tu, ni kama jana ambayo imekwisha pita; kwako ni kama mkesha mmoja wa usiku!

Zaburi 90:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi. Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu. Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu. Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku.
Zaburi 90:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi. Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu. Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu. Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku.
Zaburi 90:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Bwana, wewe umekuwa makao yetu katika vizazi vyote. Kabla ya kuzaliwa milima au hujaumba dunia na ulimwengu, wewe ni Mungu tangu milele hata milele. Huwarudisha watu mavumbini, ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.” Kwa maana kwako miaka elfu ni kama siku moja iliyokwisha pita, au kama kesha la usiku.