Zaburi 9:1-3
Zaburi 9:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Nitakushukuru Mungu kwa moyo wangu wote; nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu. Nitafurahi na kushangilia kwa sababu yako; nitaliimbia sifa jina lako, ewe Mungu Mkuu. Wakati ulipotokea, maadui zangu walirudi nyuma, walijikwaa na kuangamia.
Zaburi 9:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu; Nitafurahi na kukushangilia; Nitaliimbia sifa jina lako, Wewe Uliye juu. Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma; Hujikwaa na kuangamia mbele zako.
Zaburi 9:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu; Nitafurahi na kukushangilia Wewe; Nitaliimbia jina lako, Wewe Uliye juu. Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma; Hujikwaa na kuangamia mbele zako.
Zaburi 9:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee BWANA, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu. Nitafurahi na kushangilia ndani yako. Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana. Adui zangu wamerudi nyuma, wamejikwaa na kuangamia mbele zako.