Zaburi 86:8-13
Zaburi 86:8-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Bwana, hakuna Mungu aliye kama wewe; hakuna awezaye kufanya unayofanya wewe. Mataifa yote uliyoyaumba, yatakuja kukuabudu, ee Bwana; yatatangaza ukuu wa jina lako. Wewe ndiwe mkuu, wafanya maajabu; wewe peke yako ndiwe Mungu. Unifundishe njia yako, ee Mwenyezi-Mungu, nipate kuwa mwaminifu kwako; uongoze moyo wangu nikuheshimu. Ee Bwana, Mungu wangu, nitakusifu kwa moyo wote; nitatangaza ukuu wa jina lako milele. Fadhili zako kwangu ni nyingi mno! Umeniokoa kutoka chini kuzimu.
Zaburi 86:8-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana, Wala matendo mfano wa matendo yako. Mataifa yote uliyoyaumba watakuja; Watakusujudia Wewe, Bwana, Watalitukuza jina lako; Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, Wewe ndiwe mfanya miujiza, Ndiwe Mungu peke yako. Ee BWANA, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako; Nitakusifu Wewe, Ee Bwana, Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote, Nitalitukuza jina lako milele. Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.
Zaburi 86:8-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana, Wala matendo mfano wa matendo yako. Mataifa yote uliowafanya watakuja; Watakusujudia Wewe, Bwana, Watalitukuza jina lako; Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, Wewe ndiwe mfanya miujiza, Ndiwe Mungu peke yako. Ee BWANA, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako; Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote, Nitalitukuza jina lako milele. Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.
Zaburi 86:8-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee Bwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe, hakuna matendo ya kulinganishwa na yako. Ee Bwana, mataifa yote uliyoyafanya yatakuja na kuabudu mbele zako; wataliletea utukufu jina lako. Kwa maana wewe ni mkuu, na unafanya mambo ya ajabu; wewe peke yako ndiwe Mungu. Ee BWANA, nifundishe njia yako, nami nitaenda katika kweli yako; nipe moyo usiositasita, ili niweze kulicha jina lako. Ee Bwana Mungu wangu, nitakusifu kwa moyo wote; nitaliadhimisha jina lako milele. Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu; umeniokoa kutoka vilindi vya kaburi.