Zaburi 86:11-17
Zaburi 86:11-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Unifundishe njia yako, ee Mwenyezi-Mungu, nipate kuwa mwaminifu kwako; uongoze moyo wangu nikuheshimu. Ee Bwana, Mungu wangu, nitakusifu kwa moyo wote; nitatangaza ukuu wa jina lako milele. Fadhili zako kwangu ni nyingi mno! Umeniokoa kutoka chini kuzimu. Ee Mungu, watu wenye kiburi wamenikabili; kundi la watu wakatili wanataka kuniua, wala hawakujali wewe hata kidogo. Lakini wewe Bwana, ni Mungu wa rehema na huruma; wewe ni mvumilivu, mwingi wa fadhili na uaminifu. Unigeukie, unihurumie; unijalie nguvu yako mimi mtumishi wako, umwokoe mtoto wa mjakazi wako. Unioneshe ishara ya wema wako, ee Mwenyezi-Mungu, ili wale wanaonichukia waaibike, waonapo umenisaidia na kunifariji.
Zaburi 86:11-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako; Nitakusifu Wewe, Ee Bwana, Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote, Nitalitukuza jina lako milele. Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu. Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia; Kundi la watu wakatili wanataka kuniua. Wala hawakukuweka Wewe Mbele ya macho yao. Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli. Unielekee na kunifadhili mimi; Mpe mtumishi wako nguvu zako, Umwokoe mwana wa mjakazi wako. Unifanyie ishara ya wema, Wanichukiao waione na kuaibishwa. Kwa kuwa Wewe, BWANA, Umenisaidia na kunifariji.
Zaburi 86:11-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako; Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote, Nitalitukuza jina lako milele. Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu. Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia; Mkutano wa wakatili wamenitafuta roho. Wala hawakukuweka Wewe Mbele ya macho yao. Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli. Unielekee na kunifadhili mimi; Mpe mtumishi wako nguvu zako, Umwokoe mwana wa mjakazi wako. Unifanyie ishara ya wema, Wanichukiao waione na kuaibishwa. Kwa kuwa Wewe, BWANA, Umenisaidia na kunifariji.
Zaburi 86:11-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee BWANA, nifundishe njia yako, nami nitaenda katika kweli yako; nipe moyo usiositasita, ili niweze kulicha jina lako. Ee Bwana Mungu wangu, nitakusifu kwa moyo wote; nitaliadhimisha jina lako milele. Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu; umeniokoa kutoka vilindi vya kaburi. Ee Mungu, wenye majivuno wananishambulia; kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu: watu wasiokuheshimu wewe. Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu. Nigeukie na unihurumie; mpe mtumishi wako nguvu zako, mwokoe mwana wa mjakazi wako. Nipe ishara ya wema wako, ili adui zangu waione nao waaibishwe, kwa kuwa wewe, Ee BWANA, umenisaidia na kunifariji.