Zaburi 86:1-4
Zaburi 86:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Unitegee sikio, ee Mwenyezi-Mungu, unijibu, maana mimi ni fukara na mnyonge. Uyahifadhi maisha yangu maana mimi ni mchaji wako; uniokoe mimi mtumishi wako ninayekutegemea. Wewe ni Mungu wangu; basi, unionee huruma, maana nakulilia mchana kutwa. Uifurahishe roho yangu mimi mtumishi wako, maana sala zangu nazielekeza kwako ee Bwana.
Zaburi 86:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, utege sikio lako unijibu, Maana mimi ni maskini na mhitaji. Unihifadhi nafsi yangu, Maana mimi ni mcha Mungu. Wewe uliye Mungu wangu, Umwokoe mtumishi wako anayekutumaini. Wewe, Bwana, unifadhili, Maana nakulilia Wewe mchana kutwa. Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako, Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana.
Zaburi 86:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, utege sikio lako unijibu, Maana mimi ni maskini na mhitaji Unihifadhi nafsi yangu, Maana mimi ni mcha Mungu. Wewe uliye Mungu wangu, Umwokoe mtumishi wako anayekutumaini. Wewe, Bwana, unifadhili, Maana nakulilia Wewe mchana kutwa. Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako, Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana.
Zaburi 86:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee BWANA, sikia na unijibu, kwa maana mimi ni maskini na mhitaji. Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako, wewe ni Mungu wangu, mwokoe mtumishi wako anayekutumaini. Ee Bwana, nihurumie mimi, kwa maana ninakuita mchana kutwa. Mpe mtumishi wako furaha, kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana, ninainua nafsi yangu.