Zaburi 81:4-7 - Compare All Versions
Zaburi 81:4-7 BHN (Biblia Habari Njema)
Hiyo ndiyo kanuni katika Israeli; hilo ndilo agizo la Mungu wa Yakobo. Aliwapa watu wa Israeli agizo hilo, alipoishambulia nchi ya Misri. Nasikia sauti nisiyoitambua ikisema: “Mimi nilikutua mizigo yako mabegani, nilikuondolea matofali uliyochukua mikononi. Ukiwa shidani uliniita, nami nikakuokoa. Nilikujibu nikiwa mafichoni katika ngurumo. Nilikujaribu kwenye maji ya Meriba.
Zaburi 81:4-7 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana ni sheria kwa Israeli, Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo. Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu, Alipoondoka juu ya nchi ya Misri; Maneno yake nisiyemjua niliyasikia. Nimeutua mzigo begani mwake; Mikono yake nikaiondolea kazi nzito. Katika shida uliniita nikakuokoa; Nilikuitikia kutoka maficho yangu ya radi; Nilikujaribu penye maji ya Meriba.
Zaburi 81:4-7 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana ni sheria kwa Israeli, Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo. Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu, Alipoondoka juu ya nchi ya Misri; Maneno yake nisiyemjua naliyasikia. Nimelitenga bega lake na mzigo, Mikono yake ikaachana na kikapu. Katika shida uliniita nikakuokoa; Nalikuitikia katika sitara ya radi; Nalikujaribu penye maji ya Meriba.
Zaburi 81:4-7 NEN (Neno)
hii ni amri kwa Israeli, agizo la Mungu wa Yakobo. Aliiweka iwe kama sheria kwa Yusufu alipotoka dhidi ya Misri, huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa. Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao; mikono yao iliwekwa huru kutoka kwa kikapu. Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa, nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo; nilikujaribu katika maji ya Meriba.