Zaburi 81:1-3
Zaburi 81:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwimbieni kwa sauti Mungu, nguvu yetu, mshangilieni Mungu wa Yakobo; vumisheni wimbo wa shangwe, pigeni ngoma, chezeni zeze na kinubi cha sauti nzuri. Pigeni tarumbeta kutangaza mwezi mwandamo, na pia mwezi mpevu, wakati wa sikukuu yetu.
Zaburi 81:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo. Pazeni zaburi, pigeni matari, Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda. Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Kukiwa na mbalamwezi, wakati wa sikukuu yetu.
Zaburi 81:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo. Pazeni zaburi, pigeni matari, Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda. Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu.
Zaburi 81:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu; mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo! Anzeni wimbo, pigeni matari, pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri. Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume wakati wa Mwandamo wa Mwezi, na wakati wa mwezi mpevu, katika siku ya Sikukuu yetu