Zaburi 8:1-3
Zaburi 8:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu, kweli jina lako latukuka duniani kote! Utukufu wako waenea mpaka juu ya mbingu! Kwa sifa za watoto wadogo na wanyonyao, umejiwekea ngome dhidi ya adui zako, uwakomeshe waasi na wapinzani wako. Nikiangalia mbingu, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizozisimika huko
Zaburi 8:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni; Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mjilipiza kisasi. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha
Zaburi 8:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wewe, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni; Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha
Zaburi 8:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee BWANA, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote! Umeuweka utukufu wako juu ya mbingu. Midomoni mwa watoto wachanga na wanaonyonya umeamuru sifa, kwa sababu ya watesi wako, kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha