Zaburi 79:1-7
Zaburi 79:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mungu, watu wasiokujua wameivamia nchi yako. Wamelitia najisi hekalu lako takatifu, na kuufanya mji wa Yerusalemu kuwa magofu. Wameacha maiti za watumishi wako ziliwe na ndege, miili ya watu wako chakula cha wanyama wa porini. Damu yao imemwagwa kama maji mjini Yerusalemu, wamelazwa humo na hakuna wa kuwazika. Tumekuwa aibu kwa mataifa ya jirani, jirani zetu wanatucheka na kutudhihaki. Ee Mwenyezi-Mungu, je, utakasirika hata milele? Hasira yako ya wivu itawaka kama moto hata lini? Uwamwagie watu wasiokujua hasira yako; naam, tawala zote zisizoheshimu jina lako. Maana wamemmeza Yakobo, taifa lako, wameteketeza kabisa makao yake.
Zaburi 79:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako, Wamelinajisi hekalu lako takatifu. Wamefanya Yerusalemu chungu chungu. Wameziacha maiti za watumishi wako Ziwe chakula cha ndege wa angani. Na miili ya watauwa wako Iwe chakula cha wanyama wa nchi. Wamemwaga damu yao kama maji Pande zote za Yerusalemu, Wala hapakuwa na mtu wa kuwazika. Tumekuwa lawama kwa jirani zetu, Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka. Ee BWANA, hadi lini? Utaona hasira milele? Wivu wako utawaka kama moto? Ukali wako uwamwagie mataifa wasiokujua, Na falme za hao wasioliitia jina lako. Kwa maana wamemla Yakobo, Na makao yake wameyaharibu.
Zaburi 79:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako, Wamelinajisi hekalu lako takatifu. Wamefanya Yerusalemu chungu chungu. Wameziacha maiti za watumishi wako Ziwe chakula cha ndege wa angani. Na miili ya watauwa wako Iwe chakula cha wanyama wa nchi. Wamemwaga damu yao kama maji Pande zote za Yerusalemu, Wala hapakuwa na mzishi. Tumekuwa lawama kwa jirani zetu, Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka. Ee BWANA, hata lini? Utaona hasira milele? Wivu wako utawaka kama moto? Ukali wako uwamwagie mataifa wasiokujua, Na falme za hao wasioliitia jina lako. Kwa maana wamemla Yakobo, Na matuo yake wameyaharibu.
Zaburi 79:1-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako, wamelinajisi Hekalu lako takatifu, wameifanya Yerusalemu kuwa magofu. Wametoa maiti za watumishi kuwa chakula cha ndege wa angani na nyama ya watakatifu wako kwa wanyama wa nchi. Wamemwaga damu kama maji kuzunguka Yerusalemu yote, wala hakuna yeyote wa kuwazika. Tumekuwa kitu cha aibu kwa majirani zetu, cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka. Hata lini, Ee BWANA? Je, wewe utakasirika milele? Wivu wako utawaka kama moto hadi lini? Mwaga ghadhabu yako kwa mataifa yasiyokukubali, juu ya falme za hao wasioliitia jina lako, kwa maana wamemrarua Yakobo na kuharibu nchi ya makao yake.