Zaburi 71:10-13
Zaburi 71:10-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana maadui zangu wanasema vibaya juu yangu; wanaovizia uhai wangu wanafanya mipango, na kusema: “Mungu amemwacha; mfuateni na kumkamata, kwani hakuna wa kumwokoa!” Usikae mbali nami, ee Mungu; uje haraka kunisaidia, ee Mungu wangu. Wapinzani wangu wote waaibishwe na kuangamizwa; wenye kutaka kuniumiza wapate aibu na fedheha.
Zaburi 71:10-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana adui zangu wananiamba, Nao wanaotaka kuniua hushauriana. Wakisema, Mungu amemwacha, Mfuatieni, mkamateni, hakuna wa kumponya. Ee Mungu, usiwe mbali nami; Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia. Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.
Zaburi 71:10-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana adui zangu wananiamba, Nao wanaoniotea roho yangu hushauriana. Wakisema, Mungu amemwacha, Mfuatieni, mkamateni, hakuna wa kumponya. Ee Mungu, usiwe mbali nami; Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia. Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.
Zaburi 71:10-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa maana adui zangu wananisengenya, wale wanaonivizia kuniua wafanya hila. Wanasema, “Mungu amemwacha, mkimbilieni mkamkamate, kwani hakuna wa kumwokoa.” Ee Mungu, usiwe mbali nami, njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu. Washtaki wangu na waangamie kwa aibu, wale wanaotaka kunidhuru na wafunikwe kwa dharau na fedheha.