Zaburi 70:1-5
Zaburi 70:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Upende kuniokoa ee Mungu! Ee Mwenyezi-Mungu, uje haraka kunisaidia. Wanaonuia kuniangamiza, na waaibike na kufedheheka! Hao wanaotamani niumie, na warudi nyuma na kuaibika. Hao wanaonisimanga, na wapumbazike kwa kushindwa kwao. Lakini wote wale wanaokutafuta, wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mungu ni mkuu!” Nami niliye maskini na fukara, unijie haraka, ee Mungu! Ndiwe msaada wangu na mkombozi wangu; ee Mwenyezi-Mungu, usikawie!
Zaburi 70:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, uniokoe, Ee BWANA, unisaidie hima. Waaibike, wafedheheke, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu. Warudi nyuma, na iwe aibu yao, Wanaosema, Ewe! Ewe! Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu. Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee BWANA, usikawie.
Zaburi 70:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, uniokoe, Ee BWANA, unisaidie hima. Waaibike, wafedheheke, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu. Warudi nyuma, na iwe aibu yao, Wanaosema, Ewe! Ewe! Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu. Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee BWANA, usikawie.
Zaburi 70:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa; Ee BWANA, njoo hima unisaidie. Wale wanaotafuta kuniua, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu. Wale wanaoniambia, “Aha! Aha!” na warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao. Lakini wote wanaokutafuta washangilie na kukufurahia, wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme, “BWANA ni mkuu!” Lakini mimi bado ni maskini na mhitaji; Ee Mungu, unijie haraka. Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; Ee BWANA, usikawie.