Zaburi 7:10-17
Zaburi 7:10-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu ndiye ngao yangu; yeye huwaokoa wanyofu wa moyo. Mungu ni hakimu wa haki; kila siku hulaumu maovu. Watu wasipoongoka, Mungu atanoa upanga wake; atavuta upinde wake na kulenga shabaha. Atatayarisha silaha zake za hatari, na kuipasha moto mishale yake. Tazama! Mtu mbaya hutunga uovu, hujaa uharibifu na kuzaa udanganyifu. Huchimba shimo, akalifukua, kisha hutumbukia humo yeye mwenyewe. Uharibifu wake utamrudia yeye mwenyewe; ukatili wake utamwangukia yeye binafsi. Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwani ni mwema; nitaimba sifa za jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu.
Zaburi 7:10-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ngao yangu ina Mungu, Awaokoaye wanyofu wa moyo. Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu akasirikiaye waovu kila siku. Mtu asipoongoka ataunoa upanga wake; Ameupinda uta wake na kuuweka tayari; Naye amemtengenezea silaha za kuua, Akifanya mishale yake kuwa mipini ya moto. Tazama, huyu ametunga uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo. Amechimba shimo, amelichimba chini sana, Akatumbukia katika handaki aliyoichimba! Madhara yake yatamrejea kichwani pake, Na dhuluma yake itamshukia utosini. Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la BWANA aliye juu.
Zaburi 7:10-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ngao yangu ina Mungu, Awaokoaye wanyofu wa moyo. Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu aghadhibikaye kila siku. Mtu asiporejea ataunoa upanga wake; Ameupinda uta wake na kuuweka tayari; Naye amemtengenezea silaha za kufisha, Akifanya mishale yake kuwa ya moto. Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo. Amechimba shimo, amelichimba chini sana, Akatumbukia katika handaki aliyoifanya! Madhara yake yatamrejea kichwani pake, Na dhuluma yake itamshukia utosini. Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la BWANA aliye juu.
Zaburi 7:10-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ngao yangu ni Mungu Aliye Juu Sana, anayewaokoa wanyofu wa moyo. Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu anayeghadhibika kila siku. Mtu asipotubu, Mungu ataunoa upanga wake, ataupinda na kuufunga uzi upinde wake. Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto. Yeye aliye na mimba ya uovu na anayechukua mimba ya ghasia huzaa uongo. Yeye anayechimba shimo na kulifukua hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe. Ghasia anazozianzisha humrudia mwenyewe, ukatili wake humrudia kichwani. Nitamshukuru BWANA kwa ajili ya haki yake, na nitaliimbia sifa jina la BWANA Aliye Juu Sana.