Zaburi 68:5-6
Zaburi 68:5-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baba wa yatima, mtetezi wa wajane, ni Mungu katika makao yake matakatifu. Mungu huwaweka wapweke katika jamaa, huwaongoza wafungwa wakiimba, bali waasi huishi katika nchi kame.
Shirikisha
Soma Zaburi 68Zaburi 68:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu akaaye mahali pake patakatifu, ni Baba wa yatima na mlinzi wa wajane. Mungu huwapa fukara makao ya kudumu, huwafungua wafungwa na kuwapa fanaka. Lakini waasi wataishi katika nchi kame.
Shirikisha
Soma Zaburi 68Zaburi 68:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Ni Mungu aliye katika kao lake takatifu. Mungu huwapa wapweke makao yao; Huwapa wafungwa uhuru na kuwafanikisha; Bali wakaidi huishi katika nchi kavu.
Shirikisha
Soma Zaburi 68Zaburi 68:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake takatifu. Mungu huwakalisha wapweke nyumbani; Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa; Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu.
Shirikisha
Soma Zaburi 68