Zaburi 60:1-5
Zaburi 60:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mungu, umetutupa na kutuponda, umewaka hasira, tafadhali uturudishie nguvu. Umeitetemesha nchi na kuipasua; uzibe nyufa zake kwani inabomoka. Umewatwika watu wako mateso; tunayumbayumba kama waliolewa divai. Uwape ishara wale wanaokuheshimu, wapate kuuepa mshale. Uwasalimishe hao watu uwapendao; utuokoe kwa mkono wako, na kutusikiliza.
Zaburi 60:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, umetutupa na kututawanya, Umekuwa na hasira, uturudishe tena. Umeitetemesha nchi na kuipasua, Upaponye palipobomoka, maana inatikisika. Umewaonesha watu wako mazito, Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha. Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli. Ili wapenzi wako waopolewe, Utuokoe kwa mkono wako wa kulia, utuitikie.
Zaburi 60:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, umetutupa na kututawanya, Umekuwa na hasira, uturudishe tena. Umeitetemesha nchi na kuipasua, Upaponye palipobomoka, maana inatikisika. Umewaonyesha watu wako mazito, Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha. Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli. Ili wapenzi wako waopolewe, Uokoe kwa mkono wako wa kuume, utuitikie.
Zaburi 60:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu, umekuwa na hasira; sasa turejeshe! Umetetemesha nchi na kuipasua; uiponye mavunjiko yake, kwa maana inatetemeka. Umewaonesha watu wako nyakati za kukata tamaa; umetunywesha mvinyo unaotuyumbisha. Kwa wale wanaokucha wewe, umewainulia bendera, ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde. Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa.