Zaburi 6:6-8
Zaburi 6:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Niko hoi kwa kilio cha uchungu; kila usiku nalowesha kitanda changu kwa machozi; kwa kulia kwangu naulowesha mto wangu. Macho yangu yamechoka kwa huzuni; yamefifia kwa kutaabishwa na adui. Ondokeni kwangu enyi nyote watenda maovu! Maana Mwenyezi-Mungu amesikia kilio changu.
Zaburi 6:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakibubujikia kitanda changu; Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu. Macho yangu yameharibika kwa masumbufu, Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi. Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.
Zaburi 6:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza kitanda changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu. Jicho langu limeharibika kwa masumbufu, Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi. Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.
Zaburi 6:6-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni; usiku kucha natiririsha kitanda changu kwa machozi; nimelowesha kiti changu kwa machozi yangu. Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika, yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote. Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, kwa maana BWANA amesikia kulia kwangu.