Zaburi 6:1-4
Zaburi 6:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako; usiniadhibu kwa ghadhabu yako. Unihurumie, ee Mwenyezi-Mungu, nimeishiwa nguvu; uniponye, ee Mwenyezi-Mungu, nataabika mpaka mifupani. Ninahangaika sana rohoni mwangu. Ee Mwenyezi-Mungu, utakawia mpaka lini? Unigeukie, ee Mwenyezi-Mungu, uniokoe; unisalimishe kwa sababu ya fadhili zako.
Zaburi 6:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako. BWANA, unifadhili, maana ninanyauka; BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika. Na nafsi yangu imefadhaika sana; Na Wewe, BWANA, hadi lini? BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
Zaburi 6:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako. BWANA, unifadhili, maana ninanyauka; BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika. Na nafsi yangu imefadhaika sana; Na Wewe, BWANA, hata lini? BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
Zaburi 6:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee BWANA, usinikemee katika hasira yako, wala usiniadhibu katika ghadhabu yako. Unirehemu BWANA, kwa maana nimedhoofika; Ee BWANA, uniponye, kwa maana mifupa yangu ina maumivu makali. Nafsi yangu ina uchungu mwingi. Hadi lini, Ee BWANA, hadi lini? Geuka, Ee BWANA, unikomboe, uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.