Zaburi 57:1-3
Zaburi 57:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Unihurumie, ee Mungu, unihurumie, maana kwako nakimbilia usalama. Kivulini mwa mabawa yako nitakimbilia usalama, hata hapo dhoruba ya maangamizi itakapopita. Namlilia Mungu Mkuu, Mungu anikamilishiaye nia yake. Atanipelekea msaada toka mbinguni na kuniokoa; atawaaibisha hao wanaonishambulia. Mungu atanionesha fadhili zake na uaminifu wake!
Zaburi 57:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hadi misiba hii itakapopita. Nitamwita MUNGU Aliye Juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu. Atanitumia msaada toka mbinguni na kuniokoa, Atawaaibisha wale wanaotaka kunishambulia. Mungu atazituma Fadhili zake na kweli yake.
Zaburi 57:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hata misiba hii itakapopita. Nitamwita MUNGU Aliye juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu. Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa, Atukanapo yule atakaye kunimeza. Mungu atazipeleka Fadhili zake na kweli yake
Zaburi 57:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mabawa yako nitakimbilia hadi maafa yapite. Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu anayetimiza makusudi yake kwangu. Hutumana msaada kutoka mbinguni na kuniokoa, akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake.