Zaburi 55:1-8
Zaburi 55:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mungu, tega sikio usikie sala yangu; usiangalie pembeni ninapokuomba. Unisikilize na kunijibu; nimechoshwa na lalamiko langu. Nina hofu kwa vitisho vya maadui zangu, na kwa kudhulumiwa na watu waovu. Watu waovu wananitaabisha, kwa hasira wananifanyia uhasama. Moyo wangu umejaa hofu, vitisho vya kifo vimenisonga. Natetemeka kwa hofu kubwa, nimevamiwa na vitisho vikubwa. Laiti ningekuwa na mabawa kama njiwa! Ningeruka mbali na kupata pumziko; naam, ningesafiri mbali sana, na kupata makao jangwani. Ningekimbilia mahali pa usalama, mbali na upepo mkali na dhoruba.
Zaburi 55:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, uisikilize sala yangu, Wala usijifiche nikuombapo rehema. Unisikilize na kunijibu, Nimetangatanga nikilalama na kuugua. Kwa sababu ya sauti ya adui, Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu. Kwa maana wananitupia uovu, Na kwa ghadhabu wananiudhi. Moyo wangu unaumia ndani yangu, Na hofu za mauti zimeniangukia. Hofu na tetemeko limenijia, Na hofu kubwa imeniingia. Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa, Ningeruka mbali na kustarehe. Ningekwenda zangu mbali, Ningetua jangwani. Ningefanya haraka kuzikimbia Dhoruba na tufani.
Zaburi 55:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, uisikilize sala yangu, Wala usijifiche nikuombapo rehema. Unisikilize na kunijibu, Nimetanga-tanga nikilalama na kuugua. Kwa sababu ya sauti ya adui, Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu. Kwa maana wananitupia uovu, Na kwa ghadhabu wananiudhi. Moyo wangu unaumia ndani yangu, Na hofu za mauti zimeniangukia. Hofu na tetemeko limenijia, Na hofu kubwa imenifunikiza. Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa, Ningerukia mbali na kustarehe. Ningekwenda zangu mbali, Ningetua jangwani. Ningefanya haraka kuzikimbia Dhoruba na tufani.
Zaburi 55:1-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee Mungu, sikiliza maombi yangu, wala usidharau hoja yangu. Nisikie na unijibu. Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa kwa sauti ya adui, kwa kukaziwa macho na waovu, kwa sababu wananiletea mateso juu yangu na kunitukana kwa hasira zao. Moyo wangu umejaa uchungu, hofu za mauti zimenishambulia. Woga na kutetemeka vimenizunguka, hofu kuu imenigharikisha. Nilisema, “Laiti ningekuwa na mabawa ya njiwa! Ningeruka niende mbali kupumzika. Ningetorokea mbali sana na kukaa jangwani, ningeharakisha kwenda mahali pa salama, mbali na tufani kali na dhoruba.”