Zaburi 52:1-9
Zaburi 52:1-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote. Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila. Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli. Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila. Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai. Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka; Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kufanya mali kimbilio lake. Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele. Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.
Zaburi 52:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mbona, ewe jitu, wajivunia ubaya wako dhidi ya wenye kumcha Mungu? Kila wakati unawaza maangamizi; ulimi wako ni kama wembe mkali! Unafikiria tu kutenda mabaya. Wewe wapenda uovu kuliko wema, wapenda uongo kuliko ukweli. Ewe mdanganyifu mkuu, wapenda mambo ya kuangamiza wengine. Kwa hivyo Mungu atakuangamiza milele, atakunyakua na kukuondoa nyumbani mwako; atakungoa katika nchi ya walio hai. Waadilifu wataona hayo na kuogopa, kisha watakucheka na kusema: “Tazameni yaliyompata mtu huyu! Yeye hakutaka Mungu awe kimbilio lake; bali alitegemea wingi wa mali yake, na kutafuta humo usalama wake!” Lakini mimi ni kama mzeituni mbichi, unaostawi katika nyumba ya Mungu. Nazitegemea fadhili zake milele na milele. Ee Mungu, nitakushukuru daima, kwa ajili ya mambo uliyofanya. Nitatangaza kwamba wewe ni mwema, mbele ya watu wako waaminifu.
Zaburi 52:1-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote. Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila. Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli. Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila. Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai. Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka; Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kufanya mali kimbilio lake. Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele. Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.
Zaburi 52:1-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote. Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli. Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila. Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung’oa katika nchi ya walio hai. Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka; Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kujifanya hodari kwa madhara yake. Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele. Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.
Zaburi 52:1-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya? Kwa nini unajivuna mchana kutwa, wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu? Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. Ni kama wembe mkali, ninyi mnaofanya hila. Unapenda mabaya kuliko mema, uongo kuliko kusema kweli. Unapenda kila neno lenye kudhuru, ewe ulimi wenye hila! Hakika Mungu atakushusha chini kwa maangamizi ya milele: atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu kutoka hema lako, atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai. Wenye haki wataona na kuogopa; watamcheka, wakisema, “Huyu ni yule mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, bali alitumainia wingi wa utajiri wake, na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!” Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni unaostawi katika nyumba ya Mungu, nautegemea upendo wa Mungu usiokoma milele na milele. Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda, nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema. Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.