Zaburi 52:1-5
Zaburi 52:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mbona, ewe jitu, wajivunia ubaya wako dhidi ya wenye kumcha Mungu? Kila wakati unawaza maangamizi; ulimi wako ni kama wembe mkali! Unafikiria tu kutenda mabaya. Wewe wapenda uovu kuliko wema, wapenda uongo kuliko ukweli. Ewe mdanganyifu mkuu, wapenda mambo ya kuangamiza wengine. Kwa hivyo Mungu atakuangamiza milele, atakunyakua na kukuondoa nyumbani mwako; atakungoa katika nchi ya walio hai.
Zaburi 52:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote. Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila. Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli. Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila. Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.
Zaburi 52:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote. Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli. Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila. Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung’oa katika nchi ya walio hai.
Zaburi 52:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya? Kwa nini unajivuna mchana kutwa, wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu? Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. Ni kama wembe mkali, ninyi mnaofanya hila. Unapenda mabaya kuliko mema, uongo kuliko kusema kweli. Unapenda kila neno lenye kudhuru, ewe ulimi wenye hila! Hakika Mungu atakushusha chini kwa maangamizi ya milele: atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu kutoka hema lako, atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai.