Zaburi 51:6-14
Zaburi 51:6-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Wewe wataka unyofu wa ndani; hivyo nifundishe hekima moyoni. Unitakase kwa husopo, nitakate; unioshe niwe mweupe pe. Nijaze furaha na shangwe, nifurahishe tena, mimi ambaye uliniponda. Ugeuke, usiziangalie dhambi zangu; uzifute hatia zangu zote. Uniumbie moyo safi, ee Mungu, uweke ndani yangu roho mpya na thabiti. Usinitupe mbali nawe; usiniondolee roho yako takatifu. Unifanye nifurahi tena kwa kuniokoa, utegemeze ndani yangu moyo wa utii. Hapo nitawafunza wakosefu njia yako, nao wenye dhambi watarudi kwako. Uniokoe na hatia ya umwagaji damu, ee Mungu, Mungu mwokozi wangu, nami nitaimba kwa sauti kuwa umeniokoa.
Zaburi 51:6-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanifundisha hekima kwa siri, Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu. Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya upendo. Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako. Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, Uniponye na umwagaji wa damu, Na ulimi wangu utaiimba haki yako.
Zaburi 51:6-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri, Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi. Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako. Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, Uniponye na damu za watu, Na ulimi wangu utaiimba haki yako.
Zaburi 51:6-14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hakika wewe wapendezwa na kweli inayotoka moyoni; wanifundisha hekima ndani ya moyo wangu. Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. Unipe kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda na ifurahi. Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, na uufute uovu wangu wote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu. Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu. Unirudishie furaha ya wokovu wako, unipe roho ya utii, ili initegemeze. Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watarejea kwako. Ee Mungu, Mungu uniokoaye, niokoe na hatia ya kumwaga damu, nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako.