Zaburi 51:13-17
Zaburi 51:13-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Hapo nitawafunza wakosefu njia yako, nao wenye dhambi watarudi kwako. Uniokoe na hatia ya umwagaji damu, ee Mungu, Mungu mwokozi wangu, nami nitaimba kwa sauti kuwa umeniokoa. Uniwezeshe kusema, ee Bwana, midomo yangu itangaze sifa zako. Kwa kweli wewe hupendezwi na tambiko, ama sivyo mimi ningalikutolea. Wewe huna haja na tambiko za kuteketezwa. tambiko yangu kwako ee Mungu, ni moyo mnyofu; wewe, ee Mungu, hukatai moyo mnyofu na mtiifu.
Zaburi 51:13-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako. Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, Uniponye na umwagaji wa damu, Na ulimi wangu utaiimba haki yako. Ee Bwana, uifumbue midomo yangu, Na kinywa changu kitazinena sifa zako. Maana hupendezwi na dhabihu, na kama ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa. Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
Zaburi 51:13-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako. Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, Uniponye na damu za watu, Na ulimi wangu utaiimba haki yako. Ee Bwana, uifumbue midomo yangu, Na kinywa changu kitazinena sifa zako. Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa. Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
Zaburi 51:13-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watarejea kwako. Ee Mungu, Mungu uniokoaye, niokoe na hatia ya kumwaga damu, nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako. Ee Bwana, fungua midomo yangu, na kinywa changu kitatangaza sifa zako. Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningeileta; hufurahii sadaka za kuteketezwa. Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; moyo uliovunjika wenye toba, ee Mungu, hutaudharau.