Zaburi 5:9-12
Zaburi 5:9-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Vinywani mwao hamna ukweli; mioyoni mwao wamejaa maangamizi, wasemacho ni udanganyifu wa kifo, ndimi zao zimejaa hila. Uwaadhibu kwa hatia yao ee Mungu; waanguke kwa njama zao wenyewe; wafukuze nje kwa sababu ya dhambi zao nyingi, kwa sababu wamekuasi wewe. Lakini wafurahi wote wanaokimbilia usalama kwako, waimbe kwa shangwe daima. Uwalinde wanaolipenda jina lako, wapate kushangilia kwa sababu yako. Maana wewe Mwenyezi-Mungu wawabariki waadilifu; wawakinga kwa fadhili zako kama kwa ngao.
Zaburi 5:9-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana vinywani mwao hamna uaminifu; Moyo wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi, Ulimi wao hujipendekeza. Wewe, Mungu, uwapatilize, Na waanguke kwa mashauri yao. Uwatoe nje kwa ajili ya wingi wa makosa yao, Kwa maana wamekuasi Wewe. Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga kelele za furaha daima. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia. Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.
Zaburi 5:9-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana vinywani mwao hamna uaminifu; Mtima wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi, Ulimi wao hujipendekeza. Wewe, Mungu, uwapatilize, Na waanguke kwa mashauri yao. Uwatoe nje kwa ajili ya wingi wa makosa yao, Kwa maana wamekuasi Wewe. Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia. Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.
Zaburi 5:9-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika, mioyo yao imejaa maangamizi. Koo lao ni kaburi lililo wazi, kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu. Uwatangaze kuwa wenye hatia, Ee Mungu! Hila zao ziwe anguko lao wenyewe. Wafukuzie mbali kwa sababu ya dhambi zao nyingi, kwa kuwa wamekuasi wewe. Lakini wote wanaokimbilia kwako na wafurahi, waimbe kwa shangwe daima. Ueneze ulinzi wako juu yao, ili wale wanaolipenda jina lako wapate kukushangilia. Kwa hakika, Ee BWANA, unawabariki wenye haki, unawazunguka kwa wema wako kama ngao.