Zaburi 49:6-12
Zaburi 49:6-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Watu waovu hutegemea mali zao, hujisifia wingi wa utajiri wao. Lakini binadamu hawezi kamwe kujikomboa mwenyewe; hawezi kumlipa Mungu bei ya maisha yake, maana fidia ya maisha ni kubwa mno. Hawezi kutoa kitu chochote kinachotosha, kimwezeshe aendelee kuishi daima, asipate kuonja kaburi. Yeye afahamu kuwa hata wenye hekima hufa, wapumbavu hali kadhalika na watu wajinga. Wote hao huwaachia wengine mali zao. Makaburi ni makao yao hata milele; ni makao yao vizazi hata vizazi, ingawa hapo awali walimiliki ardhi. Binadamu hatadumu katika fahari yake; atakufa tu kama mnyama.
Zaburi 49:6-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ambao wanazitumainia mali zao, Na kujisifia wingi wa utajiri wao; Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake, Wala kumlipa Mungu fidia kwa ajili ya maisha yake, (Maana fidia ya nafsi zao ina gharama, Wala hawezi kuitoa hata milele;) ndipo aishi milele asilione kaburi. Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa; Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja, Na kuwaachia wengine mali zao. Makaburi ni nyumba zao hata milele, Maskani zao vizazi hata vizazi. Japo waliwahi kuyamiliki mashamba, Kwa majina yao wenyewe. Lakini mwanadamu hadumu katika heshima, Bali amefanana na wanyama wapoteao.
Zaburi 49:6-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wa hao wanaozitumainia mali zao, Na kujisifia wingi wa utajiri wao; Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake, Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake, (Maana fidia ya nafsi zao ina gharama, Wala hana budi kuiacha hata milele;) ili aishi sikuzote asilione kaburi. Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa; Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja, Na kuwaachia wengine mali zao. Makaburi ni nyumba zao hata milele, Maskani zao vizazi hata vizazi. Hao waliotaja mashamba yao Kwa majina yao wenyewe. Lakini mwanadamu hadumu katika heshima, Bali amefanana na wanyama wapoteao.
Zaburi 49:6-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
wale wanaotegemea mali yao na kujivunia utajiri wao mwingi? Hakuna mwanadamu yeyote awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake. Fidia ya uhai ni gharama kubwa, hakuna malipo yoyote yanayotosha, ili aishi milele na asione uharibifu. Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali yao. Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao. Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye.