Zaburi 49:10-15
Zaburi 49:10-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Yeye afahamu kuwa hata wenye hekima hufa, wapumbavu hali kadhalika na watu wajinga. Wote hao huwaachia wengine mali zao. Makaburi ni makao yao hata milele; ni makao yao vizazi hata vizazi, ingawa hapo awali walimiliki ardhi. Binadamu hatadumu katika fahari yake; atakufa tu kama mnyama. Hayo ndiyo yawapatao wanaojiamini kipumbavu, ndio mwisho wa wale wanaojivunia mali zao. Wataongozwa kama kondoo hadi kuzimu, kifo kitakuwa mchungaji wao. Watashuka moja kwa moja kaburini. Miili yao itaozea huko, Kuzimu kutakuwa makao yao. Lakini Mungu ataniokoa na kuzimu. Atanisalimisha kutoka huko.
Zaburi 49:10-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa; Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja, Na kuwaachia wengine mali zao. Makaburi ni nyumba zao hata milele, Maskani zao vizazi hata vizazi. Japo waliwahi kuyamiliki mashamba, Kwa majina yao wenyewe. Lakini mwanadamu hadumu katika heshima, Bali amefanana na wanyama wapoteao. Hiyo ndiyo njia yao, ujinga wao, Nao walioko baada yao huyaridhia maneno yao. Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na kifo kitakuwa mchungaji wao; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Miili yao itaoza, kao lao ni kuzimu. Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanipokea.
Zaburi 49:10-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa; Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja, Na kuwaachia wengine mali zao. Makaburi ni nyumba zao hata milele, Maskani zao vizazi hata vizazi. Hao waliotaja mashamba yao Kwa majina yao wenyewe. Lakini mwanadamu hadumu katika heshima, Bali amefanana na wanyama wapoteao. Hiyo ndiyo njia yao, ujinga wao, Nao walioko baada yao huyaridhia maneno yao. Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na mauti itawachunga; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Umbo lao litachakaa, kao lao ni kuzimu. Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha.
Zaburi 49:10-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali yao. Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao. Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye. Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe, pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao. Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari. Lakini Mungu atakomboa uhai wangu dhidi ya kaburi; hakika atanichukua kwake.