Zaburi 46:1-7
Zaburi 46:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu; yeye ni msaada wetu daima wakati wa taabu. Kwa hiyo hatutaogopa chochote, dunia ijapoyeyuka na milima kutikisika kutoka baharini; hata kama bahari ikichafuka na kutisha, na milima ikatetemeka kwa machafuko yake. Kuna mto ambao maji yake hufurahisha mji wa Mungu, makao matakatifu ya Mungu Mkuu. Mungu yumo mjini humo, nao hauwezi kutikiswa; Mungu ataupa msaada alfajiri na mapema. Mataifa yaghadhibika na tawala zatikisika; Mungu anguruma nayo dunia yayeyuka. Mwenyezi-Mungu wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu.
Zaburi 46:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake. Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye Juu. Mungu yu katikati ya mji hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema. Mataifa yanaghadhibika na falme kutetemeka; Anatoa sauti yake, nchi inayeyuka. BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Zaburi 46:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake. Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu. Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema. Mataifa yalighadhibika, falme zikataharuki; Alitoa sauti yake, nchi ikayeyuka. BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Zaburi 46:1-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa, na milima ianguke kilindini cha bahari, hata maji yake yakinguruma na kuumuka, na milima itetemeke kwa mawimbi yake. Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu, mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi. Mungu yuko katikati yake, hautaanguka, Mungu atausaidia asubuhi na mapema. Mataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka, yeye hupaza sauti yake, dunia ikayeyuka. BWANA wa majeshi yu pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.