Zaburi 46:1-3
Zaburi 46:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
Zaburi 46:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu; yeye ni msaada wetu daima wakati wa taabu. Kwa hiyo hatutaogopa chochote, dunia ijapoyeyuka na milima kutikisika kutoka baharini; hata kama bahari ikichafuka na kutisha, na milima ikatetemeka kwa machafuko yake.
Zaburi 46:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
Zaburi 46:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
Zaburi 46:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa, na milima ianguke kilindini cha bahari, hata maji yake yakinguruma na kuumuka, na milima itetemeke kwa mawimbi yake.