Zaburi 42:2-4
Zaburi 42:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Naona kiu ya Mungu, kiu ya Mungu aliye hai. Nitafika lini kwake na kuuona uso wake? Machozi yamekuwa chakula changu mchana na usiku, waliponiambia kila siku: “Yuko wapi Mungu Wako!” Nakumbuka tena mambo haya kwa majonzi moyoni mwangu: Jinsi nilivyokwenda na umati wa watu, nikawaongoza kwenda nyumbani kwa Mungu wakipiga vigelegele vya shukrani; umati wa watu wakifanya sherehe!
Zaburi 42:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako? Nayakumbuka mambo haya kwa uchungu moyoni mwangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza hadi katika nyumba ya Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
Zaburi 42:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako. Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
Zaburi 42:2-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu usiku na mchana, huku watu wakiniambia mchana kutwa, “Yuko wapi Mungu wako?” Mambo haya nayakumbuka ninapoimimina nafsi yangu: Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu, nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu, kwa kelele za shangwe na za shukrani katikati ya umati wa watu waliosherehekea.