Zaburi 40:7-9
Zaburi 40:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndipo niliposema: “Niko tayari; ninayotakiwa kufanya yameandikwa katika kitabu cha sheria; kutimiza matakwa yako, ee Mungu wangu ni furaha yangu, sheria yako naishika kwa moyo wangu wote!” Nimesimulia habari njema za ukombozi, mbele ya kusanyiko kubwa la watu. Kama ujuavyo ee Mwenyezi-Mungu, mimi sikujizuia kuitangaza.
Zaburi 40:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (Katika gombo la kitabu nimeandikiwa,) Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu. Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa. Sikuizuia midomo yangu; Ee BWANA, unajua.
Zaburi 40:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo nimeandikiwa,) Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu. Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa. Sikuizuia midomo yangu; Ee BWANA, unajua.
Zaburi 40:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja: imeandikwa kunihusu katika kitabu. Ee Mungu wangu, natamani kuyafanya mapenzi yako; sheria yako iko ndani ya moyo wangu.” Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, sikufunga mdomo wangu, Ee BWANA, kama ujuavyo.