Zaburi 4:5-7
Zaburi 4:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Toeni tambiko zilizo sawa, na kumtumainia Mwenyezi-Mungu. Wengi husema: “Laiti tungepata tena fanaka! Utuangalie kwa wema, ee Mwenyezi-Mungu!” Lakini mimi umenijalia furaha kubwa moyoni, kuliko ya hao walio na divai na ngano kwa wingi.
Zaburi 4:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini BWANA. Wengi husema, Nani atakayetuonesha mema? BWANA, utuinulie nuru ya uso wako. Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.
Zaburi 4:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini BWANA. Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema? BWANA, utuinulie nuru ya uso wako. Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.
Zaburi 4:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Toeni dhabihu zilizo haki; mtegemeeni BWANA. Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye kutuonesha jema lolote?” Ee BWANA, tuangazie nuru ya uso wako. Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi.