Zaburi 33:1-3
Zaburi 33:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Shangilieni kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu enyi waadilifu! Kumsifu Mungu ni wajibu wa watu wanyofu. Msifuni Mwenyezi-Mungu kwa zeze; mwimbieni kwa kinubi cha nyuzi kumi. Mwimbieni wimbo mpya; pigeni kinubi vizuri na kushangilia.
Shirikisha
Soma Zaburi 33Zaburi 33:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Mshukuruni BWANA kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa. Mwimbieni wimbo mpya, Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe.
Shirikisha
Soma Zaburi 33Zaburi 33:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Soma Zaburi 33