Zaburi 3:3-7
Zaburi 3:3-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu u ngao yangu kila upande; kwako napata fahari na ushindi wangu. Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu. Nalala na kupata usingizi, naamka tena maana wewe ee Mwenyezi-Mungu wanitegemeza. Sitayaogopa maelfu ya watu, wanaonizingira kila upande. Uje ee Mwenyezi-Mungu! Niokoe ee Mungu wangu! Wewe wawavunja mataya maadui zangu wote; wawavunja meno waovu wasinidhuru.
Zaburi 3:3-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza. Sitayaogopa maelfu na maelfu ya watu, Waliojipanga Juu yangu pande zote. BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki.
Zaburi 3:3-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza. Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote. BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki.
Zaburi 3:3-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini wewe, Ee BWANA, ni ngao yangu pande zote; umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu. Ninamlilia BWANA kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu. Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana BWANA hunitegemeza. Sitaogopa makumi elfu ya adui, wanaojipanga dhidi yangu kila upande. Ee BWANA, amka! Niokoe, Ee Mungu wangu! Wapige adui zangu wote kwenye taya, vunja meno ya waovu.