Zaburi 26:1-3
Zaburi 26:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, unitetee, maana nimeishi bila hatia, nimekutumainia wewe bila kusita. Unijaribu, ee Mwenyezi-Mungu, na kunipima; uchunguze moyo wangu na akili zangu. Fadhili zako ziko mbele ya macho yangu, ninaishi kutokana na uaminifu wako.
Zaburi 26:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi. Ee BWANA, unijaribu na kunipima; Unisafishe akili yangu na moyo wangu. Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako.
Zaburi 26:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi. Ee BWANA, unijaribu na kunipima; Unisafishe mtima wangu na moyo wangu. Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako.
Zaburi 26:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee BWANA, nithibitishe katika haki, maana nimeishi maisha yasiyo na lawama; nimemtumainia BWANA bila kusitasita. Ee BWANA, unijaribu, unipime, uuchunguze moyo wangu na mawazo yangu; kwa maana upendo wako uko mbele yangu daima, nami natembea siku zote katika kweli yako.