Zaburi 20:1-5
Zaburi 20:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu akujibu uwapo taabuni; jina la Mungu wa Yakobo likulinde. Akupelekee msaada kutoka hekaluni mwake; akutegemeze kutoka mlima Siyoni. Azikumbuke sadaka zako zote; azikubali tambiko zako za kuteketezwa. Akujalie unayotamani moyoni mwako, aifanikishe mipango yako yote. Tutashangilia kwa ajili ya ushindi wako; tutatweka bendera kulitukuza jina la Mungu wetu. Mwenyezi-Mungu akutimizie maombi yako yote!
Zaburi 20:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akutumie msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kukutimizia mipango yako yote. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. BWANA akutimizie matakwa yako yote.
Zaburi 20:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. BWANA akutimizie matakwa yako yote.
Zaburi 20:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako. Na akutumie msaada kutoka patakatifu na akupatie msaada kutoka Sayuni. Na azikumbuke dhabihu zako zote, na azikubali sadaka zako za kuteketezwa. Na akujalie haja ya moyo wako, na aifanikishe mipango yako yote. Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda, tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu. BWANA na akupe haja zako zote.