Zaburi 2:7-9
Zaburi 2:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mfalme asema: “Nitatangaza azimio la Mwenyezi-Mungu. Mungu aliniambia: ‘Wewe ni mwanangu, mimi leo nimekuwa baba yako. Niombe nami nitakupa mataifa yawe urithi wako, na dunia nzima kuwa mali yako. Utawaponda kwa fimbo ya chuma; utawavunja kama chungu cha mfinyanzi!’”
Zaburi 2:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia, Wewe ni mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako. Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.
Zaburi 2:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako. Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.
Zaburi 2:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nitatangaza amri ya BWANA: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuwa Baba yako. Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako. Utawapondaponda kwa fimbo ya chuma, na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”