Zaburi 2:2-4
Zaburi 2:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Wafalme wa dunia wanajitayarisha; watawala wanashauriana pamoja, dhidi ya Mwenyezi-Mungu na mteule wake. Wanasema: “Tujiondoe katika utawala wao; tutupilie mbali minyororo yao!” Mwenyezi-Mungu atawalaye juu mbinguni, anawacheka na kuwadhihaki.
Shirikisha
Soma Zaburi 2Zaburi 2:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake, Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupa mbali nasi kamba zao. Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.
Shirikisha
Soma Zaburi 2Zaburi 2:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake, Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao. Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.
Shirikisha
Soma Zaburi 2