Zaburi 2:10-12
Zaburi 2:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Sasa enyi wafalme, tumieni busara; sikilizeni onyo hili, enyi watawala wa dunia. Mtumikieni Mwenyezi-Mungu kwa uchaji; msujudieni na kutetemeka; asije akakasirika, mkaangamia ghafla; kwani hasira yake huwaka haraka. Heri yao wote wanaokimbilia usalama kwake!
Zaburi 2:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na sasa, enyi wafalme, iweni na hekima, Enyi watawala wa dunia, mwaonywa. Mtumikieni BWANA kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka. Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi; Heri wote wanaomkimbilia.
Zaburi 2:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili, Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe. Mtumikieni BWANA kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka. Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake itawaka upesi; Heri wote wanaomkimbilia.
Zaburi 2:10-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia. Mtumikieni BWANA kwa hofu na mshangilie kwa kutetemeka. Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia.