Zaburi 2:1-4
Zaburi 2:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa nini mataifa yanafanya ghasia? Mbona watu wanafanya njama za bure? Wafalme wa dunia wanajitayarisha; watawala wanashauriana pamoja, dhidi ya Mwenyezi-Mungu na mteule wake. Wanasema: “Tujiondoe katika utawala wao; tutupilie mbali minyororo yao!” Mwenyezi-Mungu atawalaye juu mbinguni, anawacheka na kuwadhihaki.
Zaburi 2:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mbona mataifa yanafanya ghasia, Na watu kuwaza mambo ya bure? Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake, Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupa mbali nasi kamba zao. Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.
Zaburi 2:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mbona mataifa wanafanya ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili? Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake, Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao. Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.
Zaburi 2:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na makabila ya watu kula njama bure? Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya dhidi ya BWANA na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” Yeye anayetawala mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.