Zaburi 17:13-15
Zaburi 17:13-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Inuka, ee Mwenyezi-Mungu, uwakabili na kuwaporomosha. Kwa upanga uiokoe nafsi yangu kutoka kwa waovu. Kwa mkono wako, ee Mwenyezi-Mungu, uniokoe mikononi mwa watu hao, watu ambao riziki yao ni dunia hii tu. Uwajaze adhabu uliyowawekea, wapate ya kuwatosha na watoto wao, wawaachie hata na wajukuu zao. Lakini mimi nitauona uso wako, kwani ni mwadilifu; niamkapo nitajaa furaha kwa kukuona.
Zaburi 17:13-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Inuka, Ee BWANA, umkabili, umwangushe, Kwa upanga wako uniokoe nafsi yangu na mtu mbaya. Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao liko katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao, Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.
Zaburi 17:13-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, usimame, umkabili, umwinamishe, Kwa upanga wako uniokoe nafsi na mtu mbaya. Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao, Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.
Zaburi 17:13-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Inuka, Ee BWANA, pambana nao, uwaangushe, niokoe kwa upanga wako kutoka kwa waovu. Ee BWANA, mkono wako uniokoe na watu kama hawa, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao. Bali mimi nitauona uso wako katika haki; niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.