Zaburi 145:5-7
Zaburi 145:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Nitanena juu ya utukufu na fahari yako, nitayatafakari matendo yako ya ajabu. Watu watatangaza ukuu wa matendo yako ya ajabu, nami nitatangaza ukuu wako. Watatangaza sifa za wema wako mwingi, na kuimba juu ya uadilifu wako.
Zaburi 145:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu. Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako. Watasimulia juu ya ukuu wa wema wako mwingi. Na wataiimba haki yako kwa sauti.
Zaburi 145:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu. Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako. Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu. Wataiimba haki yako.
Zaburi 145:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu. Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu. Wataadhimisha wema wako mwingi, na wataimba kwa shangwe kuhusu haki yako.