Zaburi 145:17-21
Zaburi 145:17-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu katika njia zake zote; ni mwema katika matendo yake yote. Mwenyezi-Mungu yuko karibu na wote wanaomwomba, wote wanaomwomba kwa moyo mnyofu. Huwapatia mahitaji yao wote wanaomcha; husikia kilio chao na kuwaokoa. Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wanaompenda; lakini atawaangamiza waovu wote. Nitatangaza sifa za Mwenyezi-Mungu; viumbe vyote vilisifu jina lake takatifu, milele na milele.
Zaburi 145:17-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye huruma katika matendo yake yote. BWANA yuko karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu. Hutimiza matakwa ya wote wamchao, Na pia husikia kilio chao, na huwaokoa. BWANA huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza. Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA; Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu milele na milele.
Zaburi 145:17-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote. BWANA yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu. Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa. BWANA huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza. Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA; Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu milele na milele.
Zaburi 145:17-21 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. BWANA yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu. Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa. BWANA huwalinda wote wanaompenda, bali waovu wote atawaangamiza. Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu milele na milele.