Zaburi 145:15-19
Zaburi 145:15-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Viumbe vyote vinakutazama kwa hamu, nawe wavipa chakula chao kwa wakati wake. Waufumbua mkono wako kwa ukarimu, watosheleza mahitaji ya kila kiumbe hai. Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu katika njia zake zote; ni mwema katika matendo yake yote. Mwenyezi-Mungu yuko karibu na wote wanaomwomba, wote wanaomwomba kwa moyo mnyofu. Huwapatia mahitaji yao wote wanaomcha; husikia kilio chao na kuwaokoa.
Zaburi 145:15-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Macho ya watu wote yakuelekea Wewe, Nawe huwapa chakula chao wakati wake. Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake. BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye huruma katika matendo yake yote. BWANA yuko karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu. Hutimiza matakwa ya wote wamchao, Na pia husikia kilio chao, na huwaokoa.
Zaburi 145:15-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Macho ya watu wote yakuelekea Wewe, Nawe huwapa chakula chao wakati wake. Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake. BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote. BWANA yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu. Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
Zaburi 145:15-19 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Macho ya watu wote yanakutazama, nawe huwapa chakula chao wakati wake. Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai. BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. BWANA yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu. Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa.