Zaburi 139:9-12
Zaburi 139:9-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Nikiruka hadi mawio ya jua, au hata mipakani mwa bahari, hata huko upo kuniongoza; mkono wako wa kulia utanitegemeza. Kama ningeliomba giza linifunike, giza linizunguke badala ya mwanga, kwako giza si giza hata kidogo, na usiku wangaa kama mchana; kwako giza na mwanga ni mamoja.
Zaburi 139:9-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kulia utanishika. Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
Zaburi 139:9-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika. Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
Zaburi 139:9-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nikipanda juu kwa mabawa ya mapambazuko, nikikaa pande za mbali za bahari, hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti. Nikisema, “Hakika giza litanificha na nuru inayonizunguka iwe usiku,” hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utangʼaa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.