Zaburi 139:5-8
Zaburi 139:5-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Uko kila upande wangu, mbele na nyuma; waniwekea mkono wako kunilinda. Maarifa yako yapita akili yangu; ni makuu mno, siwezi kuyaelewa. Nikimbilie wapi ambako roho yako haiko? Niende wapi ambako wewe huko? Nikipanda juu mbinguni, wewe upo; nikijilaza chini kuzimu, wewe upo.
Zaburi 139:5-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako. Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, Hayadirikiki, siwezi kuyafikia. Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
Zaburi 139:5-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako. Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, Hayadirikiki, siwezi kuyafikia. Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
Zaburi 139:5-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Umenizingira nyuma na mbele; umeweka mkono wako juu yangu. Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu, ni ya juu sana kwangu kuyafikia. Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi kuwa kitanda changu, wewe uko huko.